Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.
Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.
Lengo la Mabalozi hawa ni kuhamasisha uchangiaji na kuwezesha kujenga zaidi ya hosteli 5 kati ya 30 ambazo TEA imepanga kujenga.
Katika Uzinduzi huo uliofanyika Tarehe 31/07/2012 katika hoteli ya Serena Jijini DSM katia ya mabalozi hao na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambapo ni Faraja Nyarandu pekee ndie alikosekana kutokana na kubanwa na majukumu mengine lakini alithibitisha uwepo wake katika kampeni zinazoendelea.
See the pictures below;
Mratibu wa mabalozi wa kampeni ya uchangiaji katika ujenzi wa mabweni Rebeca Gyumi ambaye ni pia ni mtangazaji wa kipindi cha fema akielezea jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanachangisha fedha za kutosha ili lengo la TEA likamilike.
Mabalozi wa kampeni ya TEA katika ujenzi wa hosteli wakiwaomba wananchi kushiriki kampeni hii kwa kuchangia kwa kutuma ujumbe CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba 15564. Katikati ni Mkurugenzi wa uhamasishaji wa TEA Seif Mohamed.
Mkurugenzi wa uhamasishaji wa Taasisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Seif Mohamed akiielezea kampeni ya kuchangia ujenzi wa hosteli 30 zitakazowahudumia wanafunzi wa kike wa sekondari 1,504 nchini katika mikoa nane huku mabalozi wa kampeni hiyo wakifuatilia mazungumzo hayo kwa umakini katika uzinduzi wa muungano wa TEA na Mabalozi hao uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini DSM.
Mabalozi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na asiyekuwepo ni Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004) ambaye alikuwa na udhulu na atakuwepo katika kampeni zinazoendelea.
Jokate Mwegelo (kulia) akielezea imani yake kwa watanzania na kuwaomba raia wanaoiombea mema nchi yetu kuguswa kama walivyoguswa wao kujituma katika kuchangia kampeni hii ambapo ujumbe mmoja wa CHANGIA TOFALI ni shilingi 250/=, Kushoto kwake ni Mwanablog maarufu na mwanamitindo Mariam Ndaba
Nancy Sumari ambaye ni Miss Tanzania 2005 na pia mrembo aliyefikia ngazi ya juu katika mashindano hayo ya urembo akielezea jinsi alivyoguswa na kuamua kujitoa kwa asilimia mia moja kusaidia kampeni hizi. Katika kampeni hii TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi bilioni 2.3
Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa katika mradi huu.
Source :TEA.
No comments:
Post a Comment