Friday, July 6, 2012

SENSA 2012 JIANDAE KUHESABIWA

 Tujiandae watu wote wa Tanzania kuhesabiwa 26/08/2012.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.
Umoja wa Mataifa unailezea Sensa ya Watu na Makazi kama ni “Mchakato mzima wa kukusanya, kuchambua, kutathmini na kuchapisha au kusambaza takwimu za kidemografia, kiuchumi na kijamii za watu wote nchini kwa muda maalumu
2. Sensa hufanyika wakati gani?
Sensa ya watu na makazi hufanyika kila baada ya miaka 10. Sensa ya 2012 itakuwa ni Sensa ya tano tangu kupatikana Uhuru.
3. Kwa nini sensa ni muhimu?
Madhumuni ya kufanya sensa ni kuhakikisha upatikanaji wa takwimu muhimu na kwa wakati kuhusiana na idadi ya watu nchini, kwa ajili ya matumizi katika maandalizi ya sera, usimamizi, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mafanikio ya programu mbalimbali za maendeleo nchini.
4. Sensa itaendeshwa kwa taratibu zipi za kisheria.
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 itafanyika kulingana na Sheria ya Takwimu Namba 1 ya mwaka 2002.
5. Madhumuni hasa ya sensa ni yapi?
Madhumuni ya kufanya sensa ni kuhakikisha upatikanaji wa takwimu muhimu na kwa wakati kuhusiana na idadi ya watu nchini, kwa ajili ya matumizi katika maandalizi ya sera, usimamizi, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mafanikio ya programu mbalimbali za maendeleo nchini
http://www.nbs.go.tz/sensa2012/

No comments:

Post a Comment