JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA
NNE
NA MTIHANI WA MAARIFA NOVEMBA, 2013 NA UPANGAJI WA
ALAMA ZA
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA (GRADE
RANGES)
UTANGULIZI
Ndugu Wanahabari,
Taarifa
hii inahusu kuanza kufanyika Mtihani wa Kidato cha Nne na Mtihani wa Maarifa
mwaka 2013; pamoja na kufafanua kuhusuutaratibu wa upangaji wa alama za matokeo
ya Mtihaniwa kidato cha Nne na Kidato cha Sita (GradeRanges).
A. Mtihani wa Kidato cha Nne na Mtihani wa Maarifa
Novemba,2013
Mtihani
wa Kidato cha Nnena Mtihani wa Maarifa mwaka 2013 unatarajiwa kufanyika nchini
kote kwa muda wa takribani siku 18 kuanzia tarehe 04-21 Novemba, 2013. Mitihani hiyo
imetanguliwa na mitihani ya vitendo ya somo la ‘Food and Nutrition’
iliyofanyika tarehe 7- 24 Oktoba, 2013.
Takwimu za Watahiniwa:
Jumla
ya watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani ni427,906 ambapokati
yao 367,399 ni
watahiniwa wa shule na 60,507 ni
watahiniwa wa Kujitegemea. Aidha waliojiandikisha kufanya mtihani wa Maarifa ni
18,214.
Idadi hiyo ya watahiniwa wote walioandikishwa mwaka 2013 ni pungufuya watahiniwa53,508 sawa na
asilimia 11.1 ikilinganishwa
na watahiniwa 481,414 walioandikishwa
kufanya mtihani huo mwaka 2012. Watahaniwa wote walioandikishwa kufanya mtihani
mwaka 2013
wamegawanyika
katika makundi matatu kama ifuatavyo:-
Watahiniwa wa shule (School Candidates):
Kati
ya watahiniwa wa shule 367,399 walioandikishwa,
wavulana ni 198,257 sawa
na asilimia 53.96 na
wasichana 169,142 sawa
na asilimia 46.04. Watahiniwa
hao wa shule wa mwaka 2013 ni pungufu ya Watahiniwa 15,195 sawa na
asilimia 3.68 ikilinganishwa
na watahiniwa wa shule 412,
594 wa
mwaka 2012. Aidha, kati ya watahiniwa hao, watahiniwa 39 ni wasioona
na watahiniwa 305 ni
wenye uono ambao huhitaji maandishi
makubwa.
Watahiniwa wa Kujitegemea (Private Candidates):
Kati
ya watahiniwa wa kujitegemea 60,507
walioandikishwa wanaume ni 30,456 sawa na
asilimia 50.33 na
wanawake 30,051 sawa
na asilimia 49.67.
Watahiniwa wa Kujitegenea walioandikishwa mwaka 2013 ni pungufu ya Watahiniwa 8,313 sawa na upungufu
wa asilimia 12.1 ikilinganishwa
na watahiniwa 68,820 walioandikishwa
mwaka 2012.
Mtihani wa Maarifa (Qualifying Test):
Jumla
ya watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa walioandikishwa ni 18,214 wakiwemo
wanaume 7,222 sawa
na asilimia 39.65 na
wanawake 10,992 sawa na asilimia 60.35. Aidha, kati
ya watahiniwa hao 01ni
mtahiniwa asiyeona.
Watahiniwa
wa Maarifa walioandikishwa mwaka 2013 ni pungufu ya watahiniwa 3,100 sawa na upungufu
wa asilimia 14.5 ikilinganishwa
na watahiniwa 21,314 walioandikishwa
mwaka 2012. Watahiniwa wote wameandikishwa katika shule/vituo vilivyotawanyika
katika Mikoa mbalimbali nchini kama ifuatavyo:-
Jumla
ya shule 4,365 zina
Watahiniwa wa Shule (School Candidates).
Watahiniwa
wa Kujitegemea (Private candidates) wameandikishwa katika vituo 923; na
Watahiniwa wa Maarifa (Qualifying Test) wameandikishwa katika vituo 636.
Hadi
sasa maandalizi na usafirishaji wa mitihani hiyo hadi ngazi ya mkoa yamekamilika.
Aidha
mikoa inaendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa kila kituo kinapata mitihani
yake kwa muda uliopangwa kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya Baraza la
Mitihani la Tanzania.
Imetolewa,
KATIBU MKUU
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
No comments:
Post a Comment