HESLB wanawakumbusha wale wote ambao hawajawasilisha fomu na kwa wale wanaoendelea na masomo kuonesha kama wataendelea kuhitaji mkopo.
Uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013 umebaini kuwepo kwa
wanafunzi wanaoendelea na masomo na wale wanaoomba kwa mara ya kwanza ambao
hawakujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao (OLAS) na pia kutowasilisha fomu za ombi.
Bodi imetoa fursa ya mwisho kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo kukamilisha maombi
ya mikopo katika kipindi cha siku kumi na nne, kuanzia tarehe 18 Julai, 2012 kupitia mtandao
kwa anuani: http://www.heslb.go.tz/ : http://olas.heslb.go.tz
. Aidha Wanafunzi wanaoendelea na masomo watakaotuma maombi yao wanatakiwa kulipa
faini
ya
Tsh. 30,000/=
kwa njia ya M-Pesa.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni 31 Julai 2012. Hakutakuwa na muda wa
ziada baada ya muda huo kupita.
KUWASILISHA FOMU ZA WAOMBAJI WAPYA
Bodi pia inawataarifu waombaji wote wa mikopo wa mara ya kwanza ambao hawakuwasilisha
fomu zao kwa wakati kutumia muda huu wa wiki mbili kuwasilisha fomu zao Bodi zikiwa na
viambatanisho vinavyohitajika. Aidha hakutakuwa na muda wa ziada wa kuwasilisha fomu hizo
baada ya tarehe Julai 31, 2012.
Waombaji ambao hawakukamilisha taratibu za maombi ya mikopo wanahimizwa kutekeleza
maelekezo haya ndani ya muda uliopangwa kama ilivyoelekezwa. Baada ya muda huo kuisha
hakutakuwa na muda wa ziada na hivyo watakaoshindwa kutekeleza hawataweza kupata
mikopo katika mwaka wa masomo
2012/2013.
Rekebisheni mambo kabla boom halijakata watu watatafutana pia mtaarifu na mwenzio.
No comments:
Post a Comment