Saturday, April 25, 2015

SHILINGI KUPOROMOKA ZIDI YA US DOLLAR

Shilingi kuporomoka dhidi ya dola na kuvuka 1$/2000TS kunasababishwa na sababu kadhaa

1) Woga wa uchaguzi na hivyo Dola nyingi kutoingia nchini (FDI etc) kusikilizia Serikali ijayo inaundwaje

2) Woga wa uchaguzi na hivyo matajiri kununua dola kwa kasi (too many Tshs chasing too few $) ili kuzificha (hoard) nje

3) kutouza mazao nje na kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje ( current account deficit)

4) Benki Kuu kutoachia $ nyingi kwenye soko kutokana na akiba ya fedha za kigeni kupungua

5) Kuongezeka kwa huduma ya Deni la Taifa ambapo malipo ni kwa fedha za kigeni kwa madeni yaliyo wiva.

Suluhisho

1) Benki Kuu kuachia $ za kutosha kwenye soko katika muda mfupi na wa kati

2) Kuongeza mauzo nje hasa ukizingatia kwa sasa 'our exports becomes cheaper vis a vis foreign exchange)

3) Malipo ya kodi ya Ongezeko la Mtaji kutoka BG ( Shell transaction ) na Ophir (Pavilion transaction ), malipo haya kwa fedha za kigeni

4) Punguza kununua vitu vya anasa kutoka nje

5) Unafuu wa huduma kwa Deni la Taifa ( Debt relief )

6) Punguza ujazo wa fedha nchini (mop tshs out)

Hivi ndivyo Mh. Zitto Z Kabwe alivyoelezea kuhusu hali halisi katika ukurasa wake wa facebook. Na nimependa  nikaona nisave hapa.

No comments:

Post a Comment