Sunday, July 21, 2013

JE,UNARAFIKI?

Mama yangu aliwahi kuniambia ''sio kila mtu unayekuwa karibu nae ni rafiki yako''
Kila mtu anamtu ambaye anahisi ni rafiki yake lakini bila kujua huyo mtu ndiyo Yuda wako.
Mara nyingi nimekuwa nikisikia kuwa akina mama au wadada hawana ''best friend'' sababu wanaogopa kuumizwa.
Siku zote mtu anakuwa karibu na wewe kwa mambo mengi mwingine anakuwa karibu na wewe kwa sababu anajua anamatatizo ambayo wewe unaweza kumsaidia,au wewe unatatizo anaweza kukusaidia.
Muheshimu na kumpenda rafiki yako wa kweli anayekuwa nawe wakati wa shida. Sababu ukiwa nacho marafiki ni wengi ukiwa huna hawapo, therefore you need to know who is there for you.

No comments:

Post a Comment