Tuesday, February 19, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 NI JANGA.



matokeo ya mwaka 2012 ni janga
- Division I - 1,641 => 0.41%
- Division II - 6,453 => 1.62%
- Division III - 15,426 => 3.88%
- Division IV - 103,327 => 26.02%
- Division 0 = 270,289 => 68.06%
 je wadau wanasemaje??

"Matokeo yaKidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri) na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la sifuri ni mwaka tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka tunasema weeee mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote. Lazima Uwajibikaji utokee.

kwanza Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko. Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na 'urgency' katika utendaji kazi.

Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wapo kidato cha nne sasa na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni jukumu letu kuiambia Serikali hapana. Tuwape Masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani itakuja nk.

Hawa watoto wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila Wilaya. Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwneye jamii na ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.

Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Kawambwa na wenzake watoke". Watoke SASA
Riston Zera Jr facebook post

"Et matokeo mabovu ni ukosefu wa mabara, vitabu huku ni kuzunguka mbuyu na kuficha ukweli kwani book-keeping,commerce,history,civics,geography,english,kiswahili ni ukosefu wa mabara upande wa pili mwalimu amefundisha nusu ya mada mwaka mzima hapa kuna ukweli na mwalimu anaefundisha ni yule aliepata pass mbili(E) huyu akuelewa form six sijui akifundishwa hizo teaching methodologies atakuwa na uwezo wa kuelewa content uwizi mtupu UKWELI SI WAKUTAFUTWA UPO WAZI TU hii ya mgomo baridi na kukaza kalamu wakati wa kusahihisha taifa litafika pale wapanga sera wanataka lifike na kutokusikia mwisho mtasikia huu ndio MTAZAMO WA LEO" Joseph Mandala. facebook post
"Walimu ni kila kitu katika maendeleo ya jamii yoyote ile sasa kama unamlazimisha mwalimu aingie darasani kwa nguvu hutaki kumsikiliza na kupata mwafaka wa matatizo yao, unaweza kuona umeshinda maana hakuna mgomo unaoonekana na kuandikwa kwenye magazeti lakini kuna ule mwingine wa kwenye friji, na siku zote wapiganapo mafahali wawili ziumiazo ni nyasi, matokeo yake tunayaona na tutaendelea kuyaona kama mfumo hautakuwa sikivu. Unaweza kumlazimisha kuli akubebee mzigo lakini huwezi kumlazimisha mwalimu afundishe. Poleni madogo mliokuwa wahanga wa matatuzo ktk sekta ya elimu. We pray for you!" Richard Zuberi

No comments:

Post a Comment