Friday, August 31, 2012

WANAFUNZI 51 UDSM WAACHIWA HURU

Wanafunzi hao  waliachiwa huru baada ya Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya  kusikilizwa na kubainisha kuwa mahakama ilikwisha toa ahirisho la mwisho Agosti 13, mwaka huu.
Mwangamila alidai kuwa waliwasiliana na mashahidi wao ambao ni askari kupitia kwa RCO wa Wilaya ya Kinondoni ,lakini aliwaambiwa  kuwa askari hao ni moja kati ya askari waliopo kwenye Sensa ambayo ni muhimu kama kesi hiyo.
Hivyo  Wakili huyo wa Serikali aliiomba mahakama itoe ahirisho lingine la mwisho  hadi Jumatatu  kwa sababu  askari hao bado  wapo kwenye Sensa ambayo inaisha Jumapili.

Wanafunzi  walioachiwa huru ni Mwambapa Elias,Evalist Elias, Baraka Monesi, Hellen Mushi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolana Wilfred, Godfrey Deogratius , Munisi Denis,Evanos Gumbi pamoja na wenzao 40.

Awali Wakili wa Serikali, Ladslaus  Komanya alidai kuwa mnamo Novemba 11 mwaka huu,  eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio halali na kusababisha uvunjifu wa amani  eneo hilo.

No comments:

Post a Comment